Na Ahmed Sagaff, Arusha
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) inazalisha mkaa unaotokana na mabaki ya majitaka yanayosafishwa katika mabwawa yao.
Akizungumza leo jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA, Mhandisi Justine Rujomba amesema mkaa huo unatokana na mradi wa kusafisha majitaka unaogharimu shilingi bilioni 15.
"Mkaa huo hauna harufu na unaweza kutumika kwa matumizi ya kawaida," ameeleza Mhandisi Rujomba.
Pamoja na hilo, amesema mabaki mengine ya majitaka ya kutoka viwandani yatatumika kutengeneza mbolea kwa ajili ya Kilimo cha nyasi za chakula cha mifugo.
Amesema mradi huo wenye mabwawa 18 yanatopokea majitaka kutoka viwandani, una uwezo wa kutibu lita milioni 22 kwa siku na kwamba mtandao wa majitaka una kilomita 268.