Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Arusha Yapigwa Jeki Bilioni 476 kwa Ajili ya Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira.
Nov 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na. Prisca  Libaga - Arusha

WIZARA ya maji na Umwagiliaji ameitaka serikali Mkoa wa Arusha, Kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa miradi ya maji  ili kufikia mwaka 2020 lengo la serikali la kutekeleza Ilani ya CCM, kuwapatia maji safi na salama ifikiwe na hivyo kuwaondolea wananchi kero.

Rai hiyo imetolewa Oktoba 31 na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi, Isack Kamwelwe,kwenye hafla ya utiaji saini  mradi wa kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini  Arusha,wenye thamani ya shilingi bilioni 476 iliyofanyika eneo la Soko kuu jijini Arusha.

Mhandisi Kamwelwe ameitaka ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,kuhakikisha inasimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo  ili uweze kukamilika kwa wakati sanjari na kumuagiza mkandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika  kwa haraka ili uhudumie  wananchi kama ilivyokusudiwa.

Kamwelwe,amewaambia watendaji watakaosimamia  miradi hiyo ya maji  kwamba kipimo pekee  cha wao kuendeklea kubakia kazini  ni kuhakikisha miradi hiyo inakamilika  kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa .

Waziri Kamwelwe, amesema serikali inaishukuru benki ya maendeleo ya afrika AFDB, kwa kutoa mkopo wa mashariti nafuu ya Dola milioni 233,915,581sawa na shilingi bilioni 476 kwa jiji la Arusha, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika jiji la Arusha, na serikali mechangia shilingi bilioni 22,953,000.

Amesema sekta ya maji  ni miongoni mwa sekta zinazogusa maisha ya kila kiumbe duniani,na ndio maana serikali imetoa kipaumbele  kwa kugharimia miradi ya maji ili itoe huduma endelevu ya maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira  kwa wananchi .

Waziri Kamwelwe,Mchango wa sekta ya maji katika kupunguza umasikini ni pamoja  na kupunguza muda na umbali wa kwenda  kutafuta maji ili kuwezeshwa wananchi kufanya kazi zingine za maendeleo

Amesisitiza  suala la uhifadhi wa mazingira ni msingi endelevu wa upatikanaji wa maji ,uchafuzi wa vyanzo vya maji na uharibifu wa mazingira una hatari ya kusababisha janga la ukame.

Awali mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha,AUWSA,Dkt. Job Laizer, amesema kupitia mradi huo visima 56 vitachimbwa katika maeneo matano tofauti  ikiwemo Jiji la Arusha.

Amesema visima hivyo vitamaliza kabisa tatizo la upungufu wa maji na kuongeza kiwango cha uzalishaji na upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha.

Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jjiji la Arusha AUWSA, Mhandisi Ruth Koya, amesema mradi huo pia utahusisha uchumbaji wa mabwawa ya kutibu na kusafisha maji katika eneo la Themi jijini Arusha,ujenzi wa ofisi ya mamlaka ya maji.

kuongeza uzalishaji na usambazaji wa huduma ya maji kutoka lita milioni 40 kwa siku hadi lita milioni 200 na kuongeza wateja kutoka 325000 hadi kufikia wateja 600000 na kupnguza upotevu wa maji kwa asilimia 40% hadi kufikia asilimia 25% pia utahusisha ukarabati wa miundo mbinu  ya mfumo wa maji taka  kuongeza kilometa 246 za mfumo wa maji taka ,kujenga vyoo  vya kisasa kwenye  maeneo ya umma ikiwemo soko kuu na shule .

Mkurugenzi Koya,amesema kuwa kazi ya utafiti ilifanywa na kampuni ya Ufaransa julai 2016  ambayo ilibaini chanzo pekee cha kuipatia maji jiji la Arusha ni kuchimba visima virefu.

Amesema mradi huo wa kuchimba visima unatekelezwa na Kampuni ya Korea  Engineering Consltancy kwa kushirikiana na kamni ya ushauri ya wazawa ya Doutch Tanzania limited.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi