Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Arusha Waendelea Kufanya Biashara ya Maduka ya Filamu Bila Kuzingatia Sheria
Mar 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_29191" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akifafanua jambo kwa mmfanyabiashara wa Filamu Jijini Arusha walipofanya operesheni maalum kukagua bidhaa za filamu zisizofuata Taratibu na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na 4 ya mwaka 1976 mapema hivi karibuni.Katikati ni muuzaji wa duka lililobainika kujishughulisha na kazi ya kudurufu DVD za filamu za nje kinyume na sheria Bw. Innocent Msaki. Duka hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Runners Entertainment limefungiwa mpaka hapo mmiliki atakapofuata sheria.[/caption] [caption id="attachment_29192" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akifutilia kwa makini namna ambavyo mfanyabiashara wa duka la Filamu muuzaji wa duka lililobainika kujishughulisha na kudurufu DVD za filamu za nje kinyume na sheria Bw. Innocent Msaki anavyo burn DVD wakati wa operesheni maalum ya kukagua bidhaa za filamu zisizofuata Taratibu na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na 4 ya mwaka 1976 mapema wikiendi hii Jijini Arusha. Duka hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Runners Entertainment limefungiwa mpaka hapo mmiliki atakapofuata sheria.[/caption] [caption id="attachment_29193" align="aligncenter" width="1000"] Muuzaji wa duka la Runner Entertainment linalojishughulisha na kuuza Filamu kwa njia ya ku -burn DVD akifunga mlango wa duka lake kufuatia amri iliyotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania baada ya kufanyika kwa operesheni maalum ya kukagua filazu zisizofuata taratibu na sheria mapema wikiendi hii Jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_29194" align="aligncenter" width="1000"] Kutoka kulia ni Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo, Afisa Utamaduni wa Bodi hiyo Clarence Chelesi na Afisa Utamaduni wa Jiji la Arusha Maneno wakikagua Leseni katika moja ya duka linalojihusisha na biashara ya kuuza filamu wakati wa operesheni maalum ya kukagua bidhaa za filamu zisizofuata sheria na taratibu za nchi mapema wikiendi hii Jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_29195" align="aligncenter" width="1000"] Maafisa kutoka Bodi ya Filamu Tanzania, Wilhad Tairo (katikati) na Clarence Chelesi wakiwa katika operesheni maalum ya kukagua filamu zisizofuata sheria na taratibu za nchi mapema wikiendi hii Jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_29196" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Filamu Tanzania, Wilhad Tairo akikamilisha fomu ya mteja ambaye amekidhi masharti ya kupatiwa Leseni ya kuendesha biashara ya duka la Filamu wakati wa operesheni maalum ya kukagua filamu zisizofuata sheria na taratibu za nchi mapema wikiendi hii Jijini Arusha.Kulia ni Mmiliki wa duka hilo lijulikanalo kwa jina la Maandiko Shop lililopo Kata ya Levolosi Jijini Arusha Bw. Maclean David Uronu.[/caption] [caption id="attachment_29197" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Utamaduni toka Bodi ya Filamu Tanzania, Clarence Chelesi(kushoto) akimkabidhi Leseni ya kuendesha biashara ya duka la Filamu mmiliki wa duka lijulikanalo kwa jina la Maandiko Shop lililopo Kata ya Levolosi Jijini Arusha Bw. Maclean David Uronu mara baada ya kukidhi masharti na vigezo vya kupatiwa leseni hiyo mapema wikiendi hii Jijini Arusha. (Na: Mpiga Picha Wetu, Arusha)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi