Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tafiti Kusaidia Kuifikisha Tanzania Kwenye Uchumi wa Viwanda.
Aug 17, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_9310" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde akifafanua jambo kwa watafiti mbalimbali barani Afrika wakati akifungua mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Thobias Robert & Neema Mathias

Imeelezwa kuwa njia pekee ya kuifikisha Tanzania kwenye Uchumi wa kati unaochagizwa na maendeleo ya viwanda ni kwa kufanya tafiti zenye tija pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde katika uzinduzi wa mkutano wa utafiti barani Afrika ambao utadumu kwa siku tatu katika chuo cha biashara CBE, wenye lengo la kujadili viwango vya tafiti mbalimbali kwa mandeleo endelevu barani Afrika.

[caption id="attachment_9313" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akikata utepe kuzindua ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.[/caption] [caption id="attachment_9314" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akionesha ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mara baada ya kuizindua, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.[/caption]

“Falsafa ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 inahitaji uwepo wa tafiti mbalmbali, hivyo kufanyika kwa mkutano huu kutawawezesha wataalamu mbalimbali kuibua tafiti bora na zenye viwango zitakazoiwezesha Tanzania kufikia malengo yake,”alieleza Mh. Waziri Mavunde.

Aliendelea kwa kusema kuwa eneo la utafiti linapaswa kupewa kipaumbele kikubwa kwani ili kuukuza uchumi wa nchi utafiti unahitajika ili kubaini fursa za masoko, biashahara na usambazaji wa bidhaa na huduma.

Aidha alieleza kuwa watafiti wa ndani wataijifunza mambo mengi kutokana na mawasilisho mbalimbali yatakayotolewa na wageni kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo, hii itasaidia pia kubadilishana uzoefu kutoka katika nchi nyingine.

[caption id="attachment_9316" align="aligncenter" width="750"] Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu akitoa mada kwa baadhi ya watafiti wa barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa sita wa watafiti hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_9317" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu ameeleza ili nchi yoyote iweze kuendelea inahitaji kuwa na mambo makuu manne ya utafiti ambayo ni viwango, kibali, vipimo pamoja na ugenzi ambavyo huasaidia uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na viwango.

“Kwa sasa Tanzania ina mambo matatu ambayo ni viwango, ugenzi na vipimo ambavyo hufanyika katika maabara zetu hapa nchini lakini suala la kibali (Accreditation) hufanyika kikanda ambapo Tanzania hutumia kanda ya SADC kama Mwanachama wa Jumuiya hiyo.” Alifafanua Prof. Mubofu.

Prof. Mubofu alisema kuwa, viwango vya Tanzania ni bora na vinashindana na viwango vya kimataifa na katika kutengeneza bidha ili huhakikisha kuwa zinakidhi viwango vyetu na vya nchi nyingine.Pia TBS imekuwa ikiharibu bidhaa mbalimbali ambazo hutoka nchi za nje bila kuwa na viwango bora.

[caption id="attachment_9319" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika wakiendelea na mkutano mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa )[/caption]

Kwa upande  Mkuu wa chuo cha CBE unakofanyika Mkutano huo Prof. Emmanuel Mjema ameeleza kuwa tafiti na viwango kwa maendeleo endelevu zinahutajika kufanyika kwenye taasisi mbalimbali ambapo huduma zinazotolewa katika Elimu, Afya  pamoja na Kilimo zinatakiwa kuwa katika viwango bora.

“Chuo cha CBE kimekuwa kikitoa elimu na machapisho mbalimbali yenye viwango ambayo yamekuwa  yakileta faida kwa taifa letu ndiyo maana kimepata nafasi ya kuaandaa mkutano  huo unaohusisha wanataaluma mbalimbali kutoka Afrika kwa mawaka huu,” alieleza Prof Mjema.

Mkutano huu unaohusisha zaidi ya nchi 10 za bara la Afrika unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ikiwa ni mkutano wa sita tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mkutano  huo unatarajiwa kufanyika tena mwakani nchini Kenya katika chuo kikuu cha Mount Kenya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi