Makamu wa Rais Azindua Kampeni ya Upandaji Miti Rafiki ya Maji
Nov 16, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akifungua kitambaa maalum kuashiria kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, mara baada ya kupanda mti katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba, 2022. (Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selamani Jafo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Jiji la Mbeya mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos santos Silayo juu ya kuhakikisha wanazalisha miche ya kutosha ya miti rafiki wa maji kwa ajili ya upandaji wa miti hiyo nchi nzima wakati wa kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya leo tarehe 16 Novemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi na wadau wa sekta ya maji nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde unaofanyika Jijini Mbeya. Tarehe 16 Novemba, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango wa uhifadhi wa vyanzo vya maji mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabondeunaofanyika Jijini Mbeya. Tarehe 16 Novemba, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selamani Jafo