Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua lori alilolikabidhi kwa kikundi cha vijana cha Mandawa wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo, Julai 8, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo, Julai 8, 2022.