Matukio katika Picha: Utangazaji Matokeo ya Uchaguzi wa Rais, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika majimbo mbalimbali nchini ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli anaongoza kwa asilimia kubwa katika Majimbo yaliyotajwa, na kuwaacha mbali wapinzani wake, wa tatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera na wengine ni Wajumbe wa Tume hiyo, utangazaji Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kwa Kiti cha Urais unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Watazamaji wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu 2020 wakifuatilia usomwaji wa matokea ya Uchaguzi wa Rais, ambayo yanatangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mawakala wa Wagombea wa Kiti cha Urais wakifuatilia Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 katika kiti hicho ambayo ambayo yanatangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Waandishi wa Habari wakichukua habari za utangazaji matokeo ambayo yanatangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika majimbo mbalimbali nchini ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli anaongoza kwa asilimia kubwa katika Majimbo yaliyotajwa, kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera, utangazaji Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kwa Kiti cha Urais unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage, akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi(NEC), Dkt.Wilson Mahera wakati wa utangazaji matokeo ya Uchaguzi nasfasi ya Urais unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera akipanga karatasi za matokeo ambayo yamemalizwa kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji (Mst), Semistocles Kaijage, katika zoezi la utangazaji matokeo ya Uchaguzi wa Rais linalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.