Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TANESCO Toeni Bei Elekezi ya Kutandaza Nyaya Kwa Wanavijiji Kuepuka Vishoka
Oct 15, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36777" align="aligncenter" width="750"] Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Buha,wilayani Mbulu mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuwasha umeme katika baadhi ya kaya za vijiji vya wilaya hiyo.[/caption]

Na:  Zuena Msuya, Manyara.

Serikali imelika Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuweka bei elekezi kwa wakandarasi,wahandisi  na mafundi waliowaidhinisha kuwatandazia nyaya wananchi walio vijijini ili kuepusha matapeli na vishoka wanaowalaghai wananchi hao na kufanya kazi hiyo kwa gharama kubwa ukilingamisha na hadhi ya nyumba.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA) pamoja kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.

[caption id="attachment_36778" align="aligncenter" width="750"] Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika moja ya Nyumba ya mwanakijiji wa kijiji cha Buha,wilayani Mbulu mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuwasha umeme katika baadhi ya kaya za vijiji vya wilaya hiyo.[/caption] [caption id="attachment_36779" align="aligncenter" width="750"] Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Masqareda,wilayani Mbulu mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuwasha umeme katika baadhi ya kaya za vijiji vya wilaya hiyo.[/caption]

Mgalu alisema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakitozwa gharama kubwa za kutandaza nyaya katika nyumba zao kutoka kwa mafundi wanaofanya kazi hiyo licha ya gharama za kuunganishwa na umeme kuwa bei nafuu ya 27,000.

Alisema Baadhi ya mafundi wamekuwa wakiwalaghai wananchi  Kuwa hata mita namba inatakiwa kulipiwa gharama wakati wa kuwekewa hali ya kuwa mita hizo zinatolewa bure kwa wateja wote wanaounganishwa na umeme wa REA.

Aliweka wazi kuwa ni marufuku kwa mkandarasi au Fundi anayeunganishwa wateja wa umeme kupitia mradi wa REA, kumtoza mwananchi gharama za Nguzo, fomu, mita namba pamoja kifaa cha umeme tayari (UMETA) wakati utekelezaji wa mradi huo unaendelea katika eneo husika.

Aidha alirejea kusema kuwa  gharama za kuunganishwa na umeme kupitia mradi wa REA ni 27,000 tu, na endapo nyumba ya mteja inahitajika kutandazwa nyaya basi gharama hizo ni makubaliano kati ya mteja mwenyewe na Fundi, hivyo TANESCO waweke bei elekezi ili kila mteja afahamu,  gharama  kulingana na nyumba yake kuepuka matapeli.

[caption id="attachment_36780" align="aligncenter" width="750"] Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaonyesha kifaa cha umeme tayari (UMETA) , kwa wanakijiji wa kijiji Masqareda, wilayani Mbulu mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuwasha umeme katika baadhi ya kaya za vijiji vya wilaya hiyo.[/caption] [caption id="attachment_36781" align="aligncenter" width="750"] Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akicheza ngoma ya asili ya wanakijiji wa Masqareda ,wilayani Mbulu mkoani Manyara, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuwasha umeme katika baadhi ya kaya za vijiji vya wilaya hiyo.[/caption]

"Hawa vishoka na matapeli wanasababisha wananchi wasiiamini Serikali yao sikivu ya kuwahudumia wanyonge, Wengine wanaogopa kulipia gharama za kuunganishwa hasa wale wenye nyumba inayohitaji kutandazwa nyaya kutokana na gharama kubwa, kwa hali ya kawaida haiwezekani mtu anavyumba viwili au vitatu anatozwa laki nne mpaka milioni kweli jaman, TANESCO tuwasaidie wananchi wa vijijini wanufaike na umeme, na nyie wananchi wekeni mitego ya kuwamata vishoka washughulikiwe", Alisisitiza Mgalu.

Alirejea kusema kuwa wasimamizi wa REA katika utekelezaji wa mradi huo, wasikubali visingizio vitakavyotolewa na mkandarasi yeyote kwa lengo la kuchelewesha mradi huo na kwamba hakuna muda utakaoongezwa kwa mkandarasi endapo atashindwa kukamilisha kwa wakati.

Vilevile aliwasisitiza wakandarasi hao kufanya kazi kwa majibu wa mkataba uliowekwa baina yao na Serikali katika kutekeleza mradi huo ili wakamilishe kwa wakati.

Mgalu alitoa wito kwa Wakazi wa  Wilaya ya Mbulu kuwa na mahusiano mazuri, ushirikiano baina yao na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa kusambaza umeme vijijini REA katika Wilaya hiyo.

Pia vijana wajitokeze kwa wingi kufanya kazi zinazoendana na taaluma pamoja na uwezo walionao, na nipashe marufuku kwa mkandarasi yeyote kuchukuwa vijana au wafanyakazi kutoka nje ya eneo la mradi ikiwa waliopo eneo hilo wanauwezo wa kufanya kazi hizo.

Katika Kijiji cha Buha wilayani Mbulu  wateja 3 Kati ya 25 wameunganishwa na uneme na Katika Kijiji cha Masqaroda  wateja 5 Kati ya 44 Wameunganishwa ambapo zoezi LA kuwaunganisha wateja wengine litaendelea, huku wananchi wakisisitizwa kulipia huduma hiyo na kuweka tayari nyumba zao kupata huduma ya umeme.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi