Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na RasilimaliWatu Mkoa wa Katavi Bi. Crescencia Joseph akifunga mafunzo ya mifumo ya WISN na POA, Mifumo hiyo inatumika kubaini mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya na vipaumbele katika kuwapangia watumishi hao vituo vya kazi , mafunzo hayo yanayowashirikisha makatibu wa afya,maafisa utumishi,wataalamu wa takwimu za afya na waganga wakuu wa Wilaya za mkoa wa Katavi leo Jijini Mbeya.
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na RasilimaliWatu Mkoa wa Katavi Bi. Crescencia Joseph akimkabidhi Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashuri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Betueli Ruhega Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo yanayowashirikisha makatibu wa afya, maafisa utumishi, wataalamu wa takwimu za afya na waganga wakuu wa Wilaya za mkoa wa Katavi leo Jijini Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa WISN na POA yaliyofungwa leo ambapo yaliwshirikisha makatibu wa afya,maafisa utumishi, wataalamu wa takwimu za afya na waganga wakuu wa Wilaya za mkoa wa Katavi leo Jijini Mbeya.
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na RasilimaliWatu Mkoa wa Katavi Bi. Crescencia Joseph (katikati) akionesha Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo yaliyowashirikisha makatibu wa afya, maafisa utumishi, wataalamu wa takwimu za afya na waganga wakuu wa Wilaya za mkoa wa Katavi leo Jijini Mbeya.
Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashuri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Betueli Ruhega akisoma Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo yaliyowashirikisha makatibu wa afya, maafisa utumishi, wataalamu wa takwimu za afya na waganga wakuu wa Wilaya za mkoa wa Katavi leo Jijini Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na RasilimaliWatu Mkoa wa Katavi Bi. Crescencia Joseph wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo leo Jijini Mbeya.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya)