Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni June 30, 2018
May 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akijibu swali kuhusu utaratibu unaotumika kutoa ajira kwa wananchi katika sekta za Muungano leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  na Naibu Waziri Mhe. Dotto Biteko leo Bungeni  Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali  na majibu.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya hapa nchini leo  Bungeni  Jijini Dodoma.

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi ( kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,  Bunge, Uratibu,   Kazi,  Vijana,  Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.   Jenista Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni  Jijini Dodoma.

Mbunge wa Welezo  Mhe. Saada Salum  Mkuya akiuliza swali kuhusu utaratibu unaotumika katika kutoa ajira katika sekta za Muungano.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein   Mwinyi akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali  katika kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Jeshi  la Ulinzi  la Wananachi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kipindi cha maswali na majibu  leo Bungeni Jijini Dodoma.

Wanafunzi wa Shule ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo  wakati wa kipindi cha maswali na majibu, leo Jjijini Dodoma.

 

(Picha na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi