Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Balozi Mahiga Afanya Mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara wa China.
Dec 20, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25292" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi zawadi ya picha Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming mara baada ya wawili hao kufanya mazungumzo jijini beijing leo.[/caption]

Na Mwandishi Maalum, Beijing

China imeahidi kushirikiana na Tanzania kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo 2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo 2025.

Hayo yalibainishwa leo jijini Beijing  na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming na baadaye kukaririwa tena na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC), Bw. Ning Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Mahiga aliainisha na kufafanua namna Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ilivyokusudia kuwashirikisha wadau mbalimbali kwenye utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ambayo inalenga kuchochea agenda ya uchumi wa viwanda.

Miradi hiyo ni pamoja na kuendeleza nishati ya umeme ambapo Serikali imedhamiria kuzalisha umeme wa megawati 5000 ifikapo mwaka 2020 ili kuharakisha utekelezaji wa agenda ya uchumi wa viwanda ambayo haitaweza kufanikiwa kama hakutakuwa na umeme wa kutosha na wauhakika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi