[caption id="attachment_24811" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (kulia), alipokagua miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inakarabatiwa na Shirika hilo kutoka Tanga hadi Arusha, katika Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga.[/caption]
Serikali imesema imeanza kufufua reli ya Kaskazini ya kutoka Tanga hadi Arusha ambayo ilikufa miaka 14 iliyopita ili kuwezesha wafanyabiashara na wananchi kusafirisha mizigo yao kwa kutumia reli hiyo badala ya barabara hali itakayopelekea kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara nchini.
Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua ukarabati wa reli hiyo kuanzia eneo la Korogwe hadi Mombo ambalo limekamilika kwa KM 83 na kuwahikikishia watanzania kuwa uendelezaji wa reli hiyo hadi Arusha itakamilika mapema mwezi Aprili mwakani na hivyo kuruhusu huduma za usafirishaji ziendelee hasa za mazao na bidhaa. [caption id="attachment_24812" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga mara baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inatoka Tanga-Korogwe-Arusha.[/caption] [caption id="attachment_24813" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipoongea nao baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini inayotoka Tanga-Korogwe-Arusha.[/caption]"Niwahakikishie wananchi kuwa hii kazi tuliyoianza haiwezi kusimama kwani Serikali imejipanga na itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri za usafirishaji", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa, amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za reli (RAHCO), Masanja Kadogosa, kuongeza ajira kwa vijana wa maeneo hayo na kuwataka kuwa na uzalendo katika ukarabati wa reli hiyo ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia umuhimu wa kuongeza vichwa vya treni kwa Shirika hilo ambapo Serikali imeamua kununua vichwa 11 vya treni vilivyotelekezwa eneo la Bandari ya Dar es Salaam kwa kiasi cha shilingi dola milion 2.4 kutoka dola milion 3.2.
"Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kila fedha inayopatikana itasimamiwa na kuwekeza katika miundombinu ya nchi na zaidi tumeokoa dola laki nane sawa na bilioni 1.7 kwa kila kichwa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
[caption id="attachment_24814" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mombo, wilayani Korogwe, mkoani Tanga mara baada ya ukaguzi wa ukarabati wa njia ya reli ya Tanga-Korogwe-Arusha ambapo sehemu ya Tanga-Mombo KM 83 ukarabati wake umekamilika.[/caption] [caption id="attachment_24815" align="aligncenter" width="626"] Muonekano wa Reli ya Kaskazini kutoka Tanga hadi Mombo ambayo inakarabatiwa na Kampuni Hodhi ya Rasimali za Reli (RAHCO). Jumla ya KM 438 za reli ya kutokea Tanga kupitia Korogwe hadi Arusha zinatarajiwa kukarabatiwa na kukamilika mwezi Aprili mwakani.[/caption] [caption id="attachment_24816" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), leo katika Stesheni ya Mombo, mkoani Tanga, baada ya kukagua ukarabati na ufufuaji wa miundombinu ya Reli ya Kaskazini ambayo inatoka Tanga-Korogwe hadi Arusha.[/caption]Kuhusu suala la bomoabomoa katika maeneo ya hifadhi ya reli Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa ataendelea kusimamia Sheria kama inavyosema.
Prof. Mbarawa ameutaka uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), kutafuta mizigo katika viwanda vyote nchini ili kuongeza huduma za usafirishaji wa mizigo kwani ukarabati wa njia hizi za reli unahitaji fedha nyingi, hivyo upatikanaji wa mizigo hiyo utasaidia kuzalisha faida ambayo itapelekea kuongeza mapato ya Shirika hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Bw. Masanja Kadogosa, amesema kuwa ukarabati wa reli hii utakuwa na mchango mkubwa kiuchumi na kijamii kwani utasaidia kwa wananchi na wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa njia rahisi.
Ukarabati wa reli hiyo yenye urefu wa kilometa 438 ni mkakati wa Serikali katika kufufua huduma za usafiri wa treni hapa nchini na kufungua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano