Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kituo cha Afya cha Ndago Chapatiwa GaIi la Wagonjwa
Jun 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_2405" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwigulu Nchemba akiwasha gari la kubebea wagonjwa (ambulance), katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.[/caption]

Na: Nathaniel Limu- RS Singida

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa gari la kubebeba wagonjwa kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani Iramba mkoani Singida.

[caption id="attachment_2406" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa (ambulance) katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.[/caption]

Akikabidhi  gari hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amesema Gari hilo litakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na adha ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wa kituo hicho

Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ambayo iliahidi kutatua changamoto ya kero ya vifo vya wajawazito ambavyo vilikuwa vikitokea kutokana na eneo hilo kukosa gari la wagonjwa.

“Kutokana na huduma hafifu ya rufaa kwa wajawazito kwa kukosa magari ya wagonjwa, ukosefu wa damu salama na ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama, ikiwemo kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi, serikali imeona umuhimu wa kutupatia gari hili,” alisema mbunge huyo.

Aidha, aliongeza kuwa nia yake kubwa mbali na kupata msaada huo wa gari la wagonjwa pia atahakikisha anaboresha sekta ya afya katika jimbo, zahanati na vituo vyote vya afya ili kuwapa fursa wananchi wapate huduma ambayo inastahili pamoja na matibabu.

[caption id="attachment_2407" align="aligncenter" width="750"] Mkazi wa kijiji cha Urughu jimbo la Iramba mkoani Singida Jumanne Hatibu akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na serikali kupitia wizara ya afya jinsia, wazee na watoto[/caption]

Pia alisema anapambana vilivyo kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya tiba katika maeneo husika pamoja na kuongeza idadi ya wauguzi, kwani anatambua bado kuna changamoto nyingi katika sekta ya afya hivyo atajitahidi kadiri ya uwezo wake ili kuongeza kasi ya kuboresha huduma hiyo ya afya.

Awali mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ndago, Dkt Lyoce Mgelwa alisema kipindi cha nyuma wagonjwa walikuwa wanapata shida kubwa ya usafiri na wakati mwingine walishindwa kwenda kupatiwa matibabu kwa muda muafaka na kusisitiza kuwa hakuna mwananchi yeyote atakayetozwa gharama katika kutumia gari hilo.

Kwa upande wake Jumanne Hatibu mkazi wa kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago alisema kabla ya ujio wa ambulance hiyo kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa na tatizo sugu la usafiri kwa wagonjwa hasa akina mama wajawazito.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi