Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali ya Oman Yavutiwa na Mazingira ya Uwekezaji Tanzania
Nov 21, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23120" align="aligncenter" width="750"] : Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa.(Picha na: Frank Shija)[/caption]

Na: Eliphace Marwa

BALOZI wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na hatua mbalimbali znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Balozi Al Mahruqi aliyasema hayo leo aJijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.

[caption id="attachment_23121" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akizungumza jambo alipotembelewa na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula.[/caption] [caption id="attachment_23122" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Balozi Mahruqi alisema miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo upatikanaji wa tasnia ya nyama.

“Serikali ya Oman ina mpango wa kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania,” alisema   Balozi Mahruqi.

Aidha Balozi Mahruqi aliitaka Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili kuwezesha wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.

[caption id="attachment_23123" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_23124" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula(kushoto) wakimuonyesha Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi kifungu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kinachozungumzia utoaji wa huduma za jamii alipotembelea Ofisi za Naibu Waziri wa huyo leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_23125" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea Ofisi za TAMISEMI Jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula pamoja na mmoja wa Afisa kutoka Mambo ya Nje ya Nchi Bw. Odiro. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Kwa upande wake Naye Naibu  Waziri Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.

“Nitafuatilia kwa kina kwa wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo zitasaidia wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema Naibu Waziri Kakunda.

Aidha Kakunda aliahidi kufuatilia maeneo ambayo Serikali ya Oman iliahidi kusaidia kaika ujenzi wa visima mia moja vya maji katika maeneo ya mashule ili kupata orodha kamili ya shule zinazotakiwa kupatiwa msaada huo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi