Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
May 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

               Ikulu, Dar es Salaam

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 24 Mei, 2017 atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

23 Mei, 2017

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi