Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa gesi asilia inayopatikana nchini, ingali na nafasi kubwa ya kuchangia katika Pato la Taifa, tofauti na hofu ya baadhi ya watu kuwa Serikali haiipi tena kipaumbele sekta hiyo.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walizoziwasilisha katika semina maalum iliyoandaliwa na Wizara kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi asilia.
Awali, wakitoa maoni na hoja mbalimbali wakati wa semina hiyo, b...
Read More