WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa mifugo wote wa wilaya na mikoa wabadilike ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa.
“Katika ziara zangu za mikoani nimekuwa nikionesha kutoridhishwa kwangu na utendaji kazi wenu, na hasa jinsi tunavyoendesha ufugaji hapa nchini. Mmeacha kazi ya kuwaongoza wafugaji, wanafanya wanavyotaka. Tunahitaji kuona mabadiliko makubwa katika sekta hii,” amesema.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 15, 2017) wakati akizungumza na maafisa mifugo kutoka wilaya zote na mikoa yot...
Read More