Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika kesho Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai, Kilimanjaro.
Waziri Mkuu anatarajiwa kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali. Ibada ya mazishi itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni, Machame.
Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, umewasili Moshi leo ukitokea Dar...
Read More