Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Dhamana la nchi ya Sweden, (EKN), Bi. Anna-Karin Jatko, mjini Stockholm, Sweden, ambalo limetoa usaidizi katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) upande wa malighafi ya ujenzi, vitendea kazi, mifumo ya umeme, mitambo na teknolojia ambapo ameishukuru Sweden kupitia Taasisi zake likiwemo Shirika hilo la Bima la Dhamana (EKN), kwa ushirikiano wake madhubuti na kuchangia maendeleo ya Tanzania, ikiwemo ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Dar es Salaam hadi makutupora mkoani Singida.
Read More