*Akerwa na tabia ya kupokea fedha na kutopeleka vifaa, dawa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hataki kuona tabia ya kupokea fedha na kuchelewa kupeleka vifaa inayofanywa na Bohari ya Madawa (MSD) ikiendelea.
“MSD ninawatahadharisha wasirudie kosa la kupokea fedha na kutopeleka dawa na vifaa tiba. Ofisi zao ziko hapo Dodoma mjini, ni kwa nini mnachelewa kuleta vifaa hivyo,” amehoji.
Ametoa onyo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo...
Read More