Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum, akizungumza wakati akifungua kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023 katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Unguja-Zanzibar, ambapo ameitaka Kamati hiyo kuhakikisha kuwa Mkutano huo unafanyika kwa mafanikio tarajiwa pamoja na kuwanufaisha wananchi kiuchumi. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Wa Wizara ya Fedha na Mipango, Unguja-Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi pamoja na maafisa wa Serikali.
Read More