Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia samaki na boti za kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.
Read More