Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Lukuvi Akesha Akishughulikia Migogoro ya Ardhi
Jul 15, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6646" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi mida ya saa 9 usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.[/caption]

Picha/Habari na: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza  majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.

[caption id="attachment_6647" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.[/caption]

Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

[caption id="attachment_6661" align="aligncenter" width="750"] Mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam Bibi Fatuma Shami akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake kuvamiwa na kupata miliki pandikizi.[/caption] [caption id="attachment_6664" align="aligncenter" width="683"] Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani Bibi Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro.[/caption] [caption id="attachment_6666" align="aligncenter" width="750"] Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi.[/caption]

Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi