[caption id="attachment_6214" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika ukumbi waHazina Ndogo mjini Dodoma. (Picha na: OR - TAMISEMI)[/caption]
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini, kuzingatia mipaka yao ya kazi ili kuepusha migongano ya mara kwa mara pamoja na kushirikiana kwa pamoja ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi.
Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo mjini Dodoma leo katika ukumbi wa hazina ndogo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi kwaajili ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi pamoja na Wakuu wa Wilaya kutoka katika mikoa mitano ya Mara, Simiyu, Mwanza, Geita pamoja na Manyara.
“Sisi Viongozi ni kama timu ya mpira, hivyo ni lazima kila mmoja katika namba yake acheze ipasavyo ili kuleta ushindi, lakini pia pasiwepo na mtu ambaye atacheza kwa kuingilia nafasi ya mwenzie maana kwa kufanya hivyo lazima kutatokea mgongano katika utendaji kazi” Alisema.
[caption id="attachment_6223" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akiwasili katika ukumbi wa Hazina Hdogo mjini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi. Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tano.[/caption]Vilevile Mheshimiwa Simbachawene amewataka viongozi hao kwa kupitia mafunzo hayo kwenda kufanya mabadiliko ya kiutendaji kwa kuwa wabunifu ili kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kuimarisha ushirikiano baina yao wenyewe kwa wenyewe ili kutimiza lengo la pamoja la kuwaletea wananchi maendeleo.
Akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya hayo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo alizitaja mada ambazo zitatolewa kwa viongozi hao kuwa ni Mbinu za Uongozi, Majukumu na Mipaka ya Kazi, Muundo wa Serikali na namna Serikali inavyofanya kazi, Utunzaji wa Siri za Serikali pamja na Maadili katika Utumishi wa Umma.
[caption id="attachment_6224" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo yaWakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.[/caption]Mafunzo hayo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni muendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa viongozi na Wakurugenzi hao Tanzania Bara ambayo yanafanyika
kwa awamu ambapo hatimaye yatakuwa yamefanyika kwa Wakuu wa Wilaya zote Tanzania Bara.
Ufunguzi huo pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Musa Iyombe pamoja na Wakurugenzi mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI.