Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) akizungumza katika mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu uliofanyika Mkoani Singida.
Na. Mwandishi Wetu-SINGIDA
Serikali imerudisha utaratibu wa kugawa vyandarua vyenye viuatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto ikiwa nni njia moja wapo ya kupambana na ugonjwa wa malaria ambao umelkuwa ukiwaathiri sana wakina mama wajawazito na watoto.
ambao wanapatiwa chanjo ya surua kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi na mtoto ambapo utaratibu huo utaanza rasmi mwezi Agosti mwaka huu.
Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya, Bi. Epifania Malingumu alieleza ujio mpya wa Hati Punguzo wakati wa mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya muda mrefu.
Wajumbe wa mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu uliofanyika Mkoani Singida.
Alieleza kuwa kwa sasa vyandarua hiyo vitagawiwa kupitia vituo vya afya ya uzazi na mtoto tofauti na hapo awali ambapo vilikuwa vikigawiwa kupitia maduka ya mawakala.
“Utaratibu wa hati punguzo wa zamani ulikwisha muda wake mwaka 2014 ambapo wakina mama walikuwa wanapata changamoto katika kutafuta mawakala wa vyandarua lakini utaratibu mpya ni kwamba mama mjamzito au mwenye mtoto mchanga atapewa chandarua chenye viuatilifu pale pale atakapo kuwa katika kituo cha kutolea huduma za afya ya uzazi”, alieleza Bi. Malingumu.
Aidha, alifafanua kuwa takwimu zinaonesha kuwa asilimia 98 ya wajawazito huwa wanahudhuria kliniki hivyo ni rahisi kwa wajawazito hao kupata vyandarua pindi tu wanapo hudhuria kliniki na kwamba vyandarua hivyo vitatolewa kulingana na idadi ya watoto ambao mama atakua amejifungua kwa wakati huo.
Maafisa kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiutambulisha mkoani Singida mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi la ugawaji vyandarua nchini, Bw. Yusufu Mwita alieleza kuwa kwa mkoa wa Singida umekua na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa maralia kutoka asilimia 0.2 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 5.5 kwa mwaka 2016 licha ya vyandarua 954,644 kugawiwa mkoani humo kwa mwaka 2016.
Aliongeza kuwa mkakati wa ugawaji vyandarua umelenga kuwafikia asilimia 85 ya Watanzania wote ifikapo 2025 na kuutokomeza ugonjwa wa maralia kwa kushirikisha mbinu mbalimbali ikiwemo kupulizia dawa ya kuthibiti mazalia ya mbu pamoja na kuhakikisha utoaji wa matibabu sahihi ya ugonjwa wa maralia.
(Picha zote na RS-Singida)