Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Akutana na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma
Jan 24, 2019
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_39943" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam[/caption]

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

[caption id="attachment_39944" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa.[/caption]

Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

 Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini.

 Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye  utumishi wa umma.

 “Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”

 Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi