Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 5-9-2023 kwa mazungumzo na kumuaga wakielekea katika vituo vyao vya Kazi walivyopangiwa, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,ujumbe huo ukiongozwa na Balozi wa Tanzania Nchini Canada, Mhe. Balozi Joseph Sokoine (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.
Read More