Na Farida Ramadhani na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imeleeza kuwa imeshawalipa Wazabuni 2048 kiasi cha Shilingi 199 tangu kutolewa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 3 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam la kutaka Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati, aliyetaka kujua baa...