Na Mary Gwera
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania kufanya kazi kwa kiwango cha juu kwani wananchi wana matarajio makubwa na matokeo ya kazi zao.
Alisema hayo mapema Mei 07 alipokuwa akifungua Mafunzo Elekezi ya Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kituo cha Mafunzo kilichopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu-Dar es Salaam.
“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka, wakati ambao Mahakama ya Tanzania ipo katika maboresho mbalimbali, hivyo ni vye...
Read More