*Asisitiza Nia ya Kufungua Ubalozi Nchini Humo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Bi. Gladys Bejarano na kumuhakikishia ufunguzi wa ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Amesema Tanzania inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni kati yake na Cuba, hivyo inatarajia kufungua ubalozi nchini humo ili kurahisisha utendaji wa kazi za kibalozi.
Waziri Mkuu alikutana na Bi. Gladys jana jioni (Jumamosi, Agosti 26, 2017) wakati...
Read More