Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29 Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.
Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswan...
Read More