Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika, waliojadili maeneo ya kipaumbele ambayo nchi za Afrika zinahitaji kuyasukuma kama agenda mahususi katika mikutano ya Kundi la nchi 20 Tajiri Duniani (G20) baada Umoja wa Afrika kupewa kiti katika kundi hilo. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kando ya mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), jijini Washington D.C, Marekani.
Read More