Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Aprili, 2019 ameanza ziara ya kikazi ya siku 3 Mkoani Mtwara ambapo mara baada ya kuwasili ameweka jiwe la msingi katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara na kuzungumza na wananchi.
Uwanja huo unafanyiwa upanuzi ikiwa ni miaka 67 tangu ulipojengwa mwaka 1952 ambapo upanuzi unahusisha kuongeza upana wa njia ya kurukia kutoka meta 30 hadi 45, kuongeza urefu wa njia ya kurukia kutoka meta 2,258 hadi 2,800, kujenga maegesho mapya ya ndege, kujenga barabara na m...
Read More