Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Japan Tobacco Group (JT Group), Masamichi Terabatake (kulia) wakitia saini mkataba kati ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Kampuni ya Tumbaku ya Japan (JT Group) utakaoiwezesha kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma za kijamii katika maeneo inayonunua tumbaku nchini. Utiaji saini huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Septemba 11, 2023.
Read More