Na Immaculate Makilika- MAELEZO, Chato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika masuala ya uchumi kwa sababu uhusiano na urafiki wa nchi hizi mbili ni wa muda mrefu.
Hayo yamesemwa jana (Januari 8, 2020), Chato mkoani Geita, wakati Rais Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) wa kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga,...
Read More