Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa kimeacha pengo serikalini na Bungeni kwani marehemu alikuwa mchapakazi, mwadilifu na mtulivu katika utendaji kazi wake. Amesema hayo leo Jumatano (Agosti 4, 2021) alipokwenda nyumbani kwa marehemu Kwandikwa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani kutoa pole kwa familia. “Mchango wake wa utendaji katika Serikali na Bunge ni mkubwa sana alifanikiwa kuwavutia wengi kwa tabia yake ya upole, unyenyekevu na uzingatiaji...
Read More