Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi wakitia saini mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 30 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 69.9 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa kV 220, yenye urefu wa kilometa 167 kutoka Benaco hadi Kyaka pamoja na upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kyaka mkoani Kagera.
Read More