Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kuweka Mazingira Bora ya Uwekezaji
Oct 15, 2023
Serikali Kuendelea Kuweka Mazingira Bora ya Uwekezaji
Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Dotto Biteko akizungumza leo Oktoba 15, 2023, wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Mtambo Mpya wa Mabati ya Rangi kampuni ya ALAF jijini Dar es Salaam.
Na Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amewahakikishia wawekezaji nchi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wenye viwanda na wafanyabiashara ili uwekezeji wao uweze kujuza uchumi

Mhe. Biteko ameeleza hayo leo Oktoba 15, 2023, wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Mtambo Mpya wa Mabati ya Rangi kampuni ya ALAF jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, tukio hilo ni sehemu ya matunda ya juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasaan ya kuendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na pia kwa maono yake ya kuiamni sekta binafsi katika kujenga uchumi imara wa nchi.

“Napenda kuwaahidi wenye viwanda, wafanyabiashara na wawekezaji, kwamba Serikali itawapa ushirikiano. Kwa upande wenu, mnao wajibu wa kuzingatia uendelevu wa ubora na tija kulingana na viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa katika shughuli za uzalishaji hatimae kunufaika zaidi na fursa za masoko zilizopo na zinazoendelea kujitokeza,’’ ameeleza Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amewapongeza Mkurugenzi Mtendaji wa ALAF Limited, Bw. Ashish Mistry, Bodi na Menejimenti ya kiwanda cha ALAF kwa kuamua kujenga mtambo huo wa kwanza nchini na wa kisasa utakaotumika kutengeneza mabati ya rangi nchini.

“Nimeelezwa kwamba mtambo huu umegharimu jumla ya dola za Marekani milioni 25 na unatarajiwa kutoa ajira kwa watu 500. Ni dhahiri kuwa kukamilika kwake kunatoa mwelekeo mpya kwa Taifa letu kwa kuwa imekuwa ni ndoto ya nchi nyingi za Afrika kuwa na kiwanda kama hiki,” amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amesema kuzinduliwa kwa mtambo huo kunatoa fursa mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huo ikiwemo nafasi za ajira zitakazotolewa na kiwanda hicho kwa Watanzaniai kwa ujumla.

Naye, Mkurugenzi  wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman angenya amesema kuwa kiwanda hicho kimeendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora nchini jambo linalofanya wafanye vizuri katika soko.

Vile vile, Mwenyekiti wa Bodi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Bilinith Mahenge amesema kuwa kituo hicho kimeendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi