Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha Wajasiriamali wenye vitambulisho hawatozwi ushuru wala tozo nyingine yoyote inayohusiana na biashara wanazofanya na kwamba kama kuna sheria ndogo zilizokuwa zikihalalisha utozaji huo zibadilishwe.
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 12 Aprili, 2019 baada ya wananchi wa Migori Wilayani Iringa na Mtera Wilayani Mpwapwa kuusimamisha msafara wake uliokuwa ukielekea D...
Read More