Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC
Tanzania imeunga mkono uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB wa kutaka kuongezewa mtaji ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa 7 wa magavana wa ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 wanachama wa Benki hiyo, Mjini Washington DC, Marekani, Waziri wa Fedfha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndi...