WAZIRI MKUU: TUMEBAINI MADAI HEWA YA BILIONI 21/-
* Ni kwenye malipo ya mawakala wa mbolea, awali yalifikia sh. bilioni 65.
*Akiri kukutana nao, asema wenye madai halali wote watalipwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini madudu katika uhakiki wa madeni ya mawakala wa mbolea kwa sababu baadhi yao hawakuwa waaminifu.
“Tulipoanzisha mfumo wa kutoa pembeje kwa njia vocha kwa kuwatumia mawakala kupeleka pembejeo vijijini, tulibaini kuwa baadhi yao walikuwa siyo waaminifu. wakiorodhesha majina ya wakulima na kuandika kuwa wamewa...
Read More