Yasaidia wajasiriamali wadogo kwa kuwatengea sh. milioni 200 kila mwaka
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza kampuni ya TOTAL Tanzania kwa kuwekeza hapa nchini mtaji wa dola za Marekani milioni 200 (sawa na sh. bilioni 460) ndani ya miaka mitatu.
Alitoa pongezi hizo jana usiku (Alhamisi, Mei 9, 2019) kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 kwa kampuni ya TOTAL hapa nchini, zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, mabalozi, Rais wa TOTAL Africa, wakandarasi na wafanyabiashara mbali...
Read More