TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi kwa miradi 107 yenye thamani ya shilingi Bilioni 90.28 iliyobainika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu (2019) kuwa na dosari mbalimbali zikiwemo kutekelezwa chini ya ubora, kutokamilika, matumizi mabaya ya fedha za umma na udanganyifu.
Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 14 Oktoba, 2019 katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ku...
Read More