Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Prof. Ndalichako na Balozi Chassot Wakubaliana Kuimarisha Ushirikiano katika Masuala ya Kazi, Vijana na Ajira
Jul 25, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo tarehe 25 Julai, 2022, amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Kazi, Vijana, na Ajira.


Waziri Ndalichako amemuhakikishia Balozi huyo kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana naye na ameomba  kuwepo na Programu ya kuwausisha Vijana na masuala ya digitali ili waweze kutumia teknolojia kwa tija.

Naye, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Ofisi hiyo katika kuleta Maendeleo kwa Vijana hususan kupitia Programu zao za Mafunzo ya Uanagenzi.
Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Ofisi hiyo  jijini Dar es Salaam. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi