Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaji kutoka Uganda, Namibia Kuongeza Nguvu Uchunguzi Ghasia Oktoba 2025
Aug 07, 2026
Majaji kutoka Uganda, Namibia Kuongeza Nguvu Uchunguzi Ghasia Oktoba 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hasan, akizungumza wakati akizindua Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Ghasia na ukiukwaji wa sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Octoba 2025, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Na Timothy Mwaikyenda - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ushirikishwaji wa majaji kutoka nchi za Uganda na Namibia unalenga kuongeza upeo wa kitaalamu na kuimarisha uwazi, uaminifu na kuaminika kwa mchakato wa uchunguzi wa  wahusika wa ghasia na ukiukwaji wa sheria uliojitokeza nchini Oktoba 2025.

Mhe. Rais Samia amesema hayo Agosti 7, 2026 wakati akizindua rasmi Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025,  Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia Tume hiyo, Rais Samia amesema kuwa kuundwa kwa kwake kunatekeleza moja ya mapendekezo ya Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Matukio ya Ghasia na Uvunjifu wa Amani iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman, iliyowasilisha ripoti yake Aprili 23, 2026.

Aidha, Tume hiyo imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, ikiwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wa matukio ya ghasia, waliochochea vurugu hizo pamoja na waliohusika kwa namna mbalimbali, ili hatua stahiki za kisheria na kiutawala ziweze kuchukuliwa.

"Nina imani kubwa kwamba makamishna hawa watatumia taaluma, uzoefu na uadilifu wao kutekeleza jukumu hili kwa weledi mkubwa, Serikali imewapa muda wa miezi mitano kukamilisha kazi yao na endapo kutakuwa na sababu za msingi, suala la kuongeza muda litazingatiwa," amesema Rais Samia.

Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, alisema kuwa Tume hiyo imeundwa kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Jaji Mohamed Chande Othman, ambayo ilipendekeza kufanyika kwa uchunguzi wa kina zaidi kuhusu wahusika wa ghasia na ukiukwaji wa sheria uliojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Ameongeza kuwa tume hiyo ina makamishna sita wakiongozwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Shaaban Ali Lila, huku wajumbe wengine wakiwa ni Naibu Jaji Mkuu wa Namibia, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Uganda na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki,na wengine watatu kutoka Tanzania kutimiza idadi ya wajumbe sita wanaounda tume hiyo.

Huku akieleza kuwa sekretarieti ya Tume hiyo itaongozwa na Bw. Paul Kadushi na kwamba maandalizi yote ya kuanza kazi yamekamilika, huku wajumbe wote wakiwa tayari kuanza kutekeleza majukumu yao mara moja.

Kwa mujibu wa hadidu za rejea zilizotolewa na Rais, Tume hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi zake ndani ya siku 150 na kuwasilisha ripoti pamoja na mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha utawala wa sheria, uwajibikaji na amani nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor