Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Korea ya Kusini kwa Ziara ya Kikazi
Oct 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 23, 2022) kwenda Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu. 

Akiwa Korea Kusini, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Han Duck-soo. Pia anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda.

Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini. Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30.

Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi