Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Samia Japan
Sep 24, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe.

Taratibu za kutoa heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan. Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.

Bw. Abe ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

Akiwa Japan, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi