Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa NACOPHA
Sep 07, 2023
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI alipotembelea banda la Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA) katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa NACOPHA uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.
Na
Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi walioshiriki katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA) wakiimba wimbo wa taifa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Septemba 7, 2023. Baadhi ya washiriki wa Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ( NACOPHA) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.