Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Dkt. Mabula Atoa Siku 14 Halmashauri ya Serengeti Kutoa Taarifa ya Mashamba 36
Jul 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Munir Shemweta, SERENGETI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula ameipa wiki mbili Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kumpatia taarifa ya hali ya mashamba 36 yaliyopo katika halmashauri hiyo ili yale mashamba yasiyoendelezwa yaweze kubatilishwa umiliki wake.

Hatua hiyo inafuatia kuelezwa kupitia taarifa ya sekta ardhi ya halmashauri ya wilaya hiyo kuwa wilaya hiyo ina mashamba yaliyopimwa ni 36.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Afisa Ardhi Mteule wa Halmasahauri hiyo ya Serengeti, Orwaka Nyamsusa ilieleza kuwa, mashamba hayo yalipimwa vijijini bila kufuata taratibu za uhaulishaji na ilipotakiwa yamilikishwe kwa kupewa hati za kawaida ilishindikana.

"Ninawapa Serengeti wiki mbili nijue hali ya mashamba hayo na kama ni suala la kuanza kuyabatilisha, mchakato uanzie katika halmashauri ambayo ni mamlaka ya upangaji ili tuitangaze fursa kwa wawekezaji, kama Serengeti tunayo mashamba 36 na kati ya hayo ni matano tu yenye umiliki halali’’. Alisema Dkt Mabula

Akizungumza na uongozi wa wilaya hiyo na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo tarehe 12 Julai, 2022 wilayani humo, Dkt Mabula alisema haingii akilini mashamba pamoja na ardhi kuwa katika halmashauri hiyo lakini halmashauri husika haina kumbukumbu  iwapo imeyapima mashamba hayo na badala yake inaenda kutafuta kumbukumbu wizarani.

Alibainisha kuwa, kama utaratibu wa kuisimamia sekta ya ardhi hivyo kama kwa halmashauri ya Serengeti utaratibu utakuwa ni wa aina hiyo basi halmashauri hiyo haiwezi kufika popote katika masuala ya ardhi na itaendelea kuwa na changamato.

" Halmashauri ni mamlaka za upangaji kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya Mipango Miji ya 2007, ni mamlaka za upangaji zinazotakiwa kupanga miji yao wanavyotaka, wizara kazi yake ni kusimamia na kuangalia kama shughuli za ardhi zinaenda kwa utaratibu au kufuata sheria .

Alisema, halmashauri nyingi hazifuati takwa la sheria huku zikifahamu ni mamlaka za upangaji na kueleza kuwa halmashauri zote zinatakiwa kutekeleza takwa hilo na zisipotekekeza migogoro yq ardhi haiwezi kuisha.

Katika taarifa yake, halmashauri hiyo ilieleza kuwa wilaya hiyo ina jumla ya vijjji 78 ambapo kati ya hivyo vijjji 61 vimepimwa huku vijiji 10 kati ya hivyo vikitakiwa kufanyiwa marejeo kutokana na makosa katika ramani za upimaji.

Aidha, jumla ya vijiji 29 kati ya 78 vina mpango wa matumizj bora ya ardhi ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/ 2023 halmashauri hiyo imetenga kiasi cha Shilingi 15,000,000 kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji 3.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi