Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wavamizi wa Reli Wapewa Miezi Sita Kuondoka.
Jul 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_6118" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akipokea maelezo ya kifaa maalumu cha kugundua sehemu ambayo mkongo wa Taifa una tatizo kutoka kwa Bw. Juma Ngimba (Kulia), wakati alipokagua eneo ambalo Mkongo wa Taifa umeharibika kwa kuliwa na panya Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) akiangalia ramani ya Mkongo wa Taifa wakati alipokagua eneo ambalo Mkongo wa Taifa umeharibika kwa kuliwa na panya Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.[/caption]

Na. Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngoyani, ametoa miezi sita kwa wakazi wa Mpanda Mkoani Katavi kuondoka katika maeneo ya hifadhi za Reli ili kupisha maboresho yanayoendelea kufanywa na Shirika la Reli Tanzania (TRL) kwenye miundombinu yake. Ametoa agizo hilo wakati akiongea na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo mkoani Katavi na kusema wakati sasa umefika kwa wananchi kufuata Sheria kwa kutovamia miundombinu. “Ninatoa miezi sita kuanzia sasa, itakapofika wezi Januari mwakani wananchi wote watakaokuwa ndani ya hifadhi ya Reli watabomolewa nyumba zao kwa kuzingatia Sheria zinazolinda miundombinu,” alisisitiza Eng. Ngonyani. Naibu Waziri Eng. Ngonyani ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mpanda kusimamia zoezi la wananchi kuhama na kuhakikisha kila aliyevamia miundombinu hiyo anabomoa nyumba yake kabla ya Sheria kufata mkondo wake. [caption id="attachment_6127" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa Kampuni ya Simu (TTCL) mkoa wa Rukwa na Katavi Bw. Bw. Peter Kuguru (aliyenyoosha kidole) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani wakati alipokagua eneo ambalo Mkongo wa Taifa umeharibika kwa kumegwa na panya Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.[/caption] Aidha, Eng. Ngonyani amewatahadharisha wafanyakazi wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS) kuzingatia maslahi mapana ya Taifa wakati wa kutafuta zabuni kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Magufuli katika juhudi zake za kuimarisha miundombinu nchini. Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amekagua barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni (76.6KM), Sumbawanga-Kanazi (75KM) ambapo ameiagiza TANROADS Mkoa wa Rukwa kuweka mizani katika barabara zinazojengwa ili kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito na kusababisha uharibifu kwa barabara katika Mkoa huo. “Ni wakati sasa wanaotoa huduma za usafirishaji wa mizigo kufuata  Sheria na kubeba mzigo wa uzito unaostahili sababu madereva hao hao wakienda nchi za jirani wanafuata Sheria kwa umakini, SUMATRA simamieni utoaji wa leseni kwa magari ya abiria na mizigo kwa kuzingatia uzito wa magari ili kuziweshesha barabara zetu zidumu,” alisisitiza Eng. Ngonyani. [caption id="" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akipata maelezo ya juu ya mtambo wa kukuza mawimbi ya simu kutoka Meneja wa Kampuni ya Simu (TTCL) mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Bw. Peter Kuguru.[/caption] Kwa upande wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa, Eng. Msuka Mkina amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa Wakala utahakikisha Mizani inawekwa sehemu za barabara  ili kubaini Magari yanayozidisha uzito na kuyachukulia hatua za kisheria. Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi, huduma za mawasiliano ya simu   na Madaraja katika Mkoa wa Katavi na Rukwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi